Habari

Kiongozi mwenza na Odinga, Kalonzo Musyoka akataa kuapishwa

Ikiwa ni wiki mbili zimepita tangu Kiongozi wa umoja wa vyama vya upinzani nchini Kenya (NASA), Raila Odinga ajiapishe kuwa ni Rais wa watu nchini humo, hatimaye leo Makamu wake, Kalonzo Musyoka ambaye siku ya kuapishwa kwa Odinga hakuhudhuria amekanusha taarifa kuwa ataapishwa mwishoni mwa mwezi huu.

Kalonzo Musyoka

Kalonzo amesema kuwa taarifa hizo zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa ataapishwa mwishoni mwa mwezi februari, 2018 sio za kweli na hawezi kufanya hivypo kwa sababu ni kinyume na Katiba ya nchi hiyo.

Najua Ruto anasubiri niapishwe ili apate sababu za kunifungulia mashtaka ya uhaini ili kuniharibia mipango ya kugombea urais mwaka 2022 dhidi yake, Kwani kuapishwa ni tukio la kinyume na katiba ya nchi na nasisitiza sitaapishwa kama inavyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari,“amesema Msyoka leo Februari 13, 2018 alipokuwa mjini Machakos akiongea na viongozi wapya wanawake walioteuliwa na NASA.

Soma zaidi – Hatimaye Raila Odinga ajiapisha kuwa Rais wa Kenya mbele ya maelfu ya watu

Hata hivyo, kauli hiyo imewatibua maelfu ya watu nchini Kenya wengi wakimuita kuwa ni MSALITI na mtu muoga katika kupigania maslahi ya Wakenya.

https://twitter.com/IkeOjuok/status/963372897573244928

Awali Raila Odinga wakati akiapishwa kwenye Viwanja vya Uhuru Park jijini Nairobi mnamo tarehe 30 Januari 2018 aliwatangazia wafuasi wa NASA kuwa Msyoka ataapishwa hivi karibuni.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents