Habari

Kiongozi mzee zaidi achaguliwa upya kuiongoza Malaysia

Waziri Mkuu wa zamani wa Malaysia, Dkt. Mahathir Mohamad mwenye umri wa miaka 92, amefanikiwa kupata ushindi wa kihistoria duniani.

Dkt. Mahathir ambaye alikuwa Waziri Mkuu tangu mwaka 1981 hadi 2003, amepata ushindi huo kwa kumuangusha Najib Razak aliyekalia kiti hicho tangu mwaka 2009 kupitia chama cha Barisan Nasional ambacho kimekuwa madarakani tangu mwaka 1957.


Wananchi wa Malaysia wakishangilia ushindi wa Dkt. Mahathir Mohamad

Kuanguka kwa chama hiko kikongwe kwenye uchaguzi huo inatokana na kutuhumiwa kujihusisha na rushwa pamoja na ufisadi.

Wakati huo huo kushindwa kwa Razak kumedaiwa ni kutokana na tuhuma zinazomkabili za kujipatia kiasi cha dola 700 kutoka taasisi moja ya maendeleo ya Malaysia hata hivyo bado uchunguzi wa tukio hilo unaendelea.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents