Habari

Kiongozi wa jeshi wa Panama Manuel Noriega afariki dunia

Manuel Noriega ambaye alikuwa kiongozi wa kijeshi wa zamani kutoka Panama amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 83.

Kwa mujibu wa shirika la habari la CNN limesema kuwa kiongozi huyo amefariki baada ya kuvuja damu kutokana na upasuaji aliofanyiwa wa kuondoa uvimbe uliopo katika ubongo mwezi Machi mwaka huu katika hospitali ya Panama City hospital.

Awali Noriega alikuwa rafiki wa karibu wan nchi ya Marekani lakini aliondolewa madarakani kwa nguvu na wanajeshi wa Marekani walipovamia nchi yake mwaka 1989 na aliingia katika hatia ya mashtaka ya dawa ya kulevya mwaka 1991.

Mwezi Januari mwaka huu Manuel aliachiwa huru kwa ajili ya kwenda kufanyiwa upasuaji kwenye ubongo wake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents