Burudani ya Michezo Live

Kiongozi wa upinzani Malawi ashinda uchaguzi

Kiongozi wa upinzani nchini Malawi Lazarus Chakwera ameshinda uchaguzi  wa  wiki  hii  wa  rais ulioamriwa  kufanyika  tena kwa asilimia 58.57 ya kura, tume ya uchaguzi ya nchi hiyo imesema.

Malawi Opposition Lazarus Chakwera (Reuters/E, Chagara)

Ilikuwa  ni  mabadiliko  makubwa ya majaaliwa  kwa  kiongozi aliyeko madarakani, Peter Mutharika, ambaye  ushindi  wake  katika uchaguzi  wa  mwezi  Mei  2019 ulibatilishwa na mahakama  ya katiba, yakihusishwa  na  udanganyifu  mkubwa.

Kiasi ya  wapiga  kura  milioni 6.8  katika  taifa  hilo  dogo  la  kusini mwa  Afrika walijitokeza  katika  vituo vya  kupigia  kura  siku  ya Junanne. Na  jana  Jumamosi , tume  ya  mwenyekiti  wa  tume  ya uchaguzi  Chifundo Kachale aliwaambia  waandishi  habari; “Tume imemtangaza Lazarus Chakwera , kwa  kupata  asilimia 58.57 ya kura, kuwa  amechaguliwa  kuwa  rais wa  Malawi.

Malawi Präsident Peter Mutharika PK Wahlen (picture-alliance/AP Photo/T. Chikondi)

Mutharika  alikuwa  wa  pili  kwa  kupata  kura  1,751,377, wakati mgombea  ambaye  hajulikani  sana  Peter Dominico Kuwani amepata  kuwa 32,456.

Watu waliojitokeza  kupiga  kura  ni  asilimia 64.81.

Tangazo  hilo lilipokelewa  kwa  shangwe  kubwa  na  vigelegele wakati  waungaji  mkono  upinzani  wakipepea  bendera  ya  Malawi yenye rangi  nyekundu , nyeusi  na  kijani na  kuimba “serikali” katika lugha  ya  Kichechewa.

Mwezi  Februari , mahakama  ya  juu  ya  Malawi  iliona  kuwa uchaguzi  wa  kwanza  umegubikwa  na  mapungufu  mengi , ikiwa  ni pamoja  na  matumizi ya  wino wa  kufanyia  marekebisho kubadilisha  matokeo  katika  karatasi  ya  matokeo.

Ushindi kwa Wamalawi

Hukumu  hiyo ya kihistoria  imeifanya  Malawi  kuwa  nchi  ya  pili  ya Afrika  kusini  mwa  jangwa  la  Sahara  kubatilisha  matokeo  ya  rais , baada  ya  Kenya  mwaka  2017.

“Huu  ni  ushindi  kwa  Wamalawi , ni  ushindi  kwa  demokrasia , ni ushindi  kwa  haki,” amesema  Chakwera  aliyechaguliwa baada  ya ushindi  wake  kutangazwa.

“Ni  ushindi  ambao  utaliwezesha  taifa  hili kuanza  upya  na  kuanza kujenga  aina  mpya  ya  Malawi  ambayo  sisi  wote  tutahusika.”

Wakati  huo  huo , kundi  la  watu  waliokuwa  wakifurahia lilijikusanya  kufyatua  fashi fashi  katika  makao  makuu  ya  chama cha  Chakwera  cha  Malawi Congress Party katika  mji  mkuu Lilongwe.

Mutharika  hakupenda  kusema  lolote  juu  ya  kushindwa  kwake.

Mapema  jana  Jumamosi , Mutharika  alidai kuwa  uchaguzi  huo uliofanyika  tena  una mapungufu, akielezea  kuhusu  ghasia  na kutishwa  kwa  waangalizi  wa  chama  chake  cha  DPP.

“Hatuna  maelezo  zaidi  ya  kutoa,” msemaji  wa  Mutharika  Mgeme Kalilani aliliambia  shirika  la  habari  la  AFP baada  ya  matokeo. “Taarifa  tuliyotoa  mapema leo inatosha.”

Rais  huyo  anayeondoka  madarakani wa chama  cha  Democratic Progressive Party DPP siku  ya  Ijumaa  alitoa  wito  kwa  tume  ya uchaguzi  ya  Malawi  kubatilisha  matokeo  ya  kura  ya  pili na itangaze uchaguzi  wa  tatu.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW