Habari

Kiongozi wa upinzani Uganda Besigye ashtakiwa kwa uhaini

Kiongozi wa upinzani nchini Uganda,  Kizza Besigye ameshtakiwa kwa kosa la uhaini baada ya kujitangaza mshindi wa uchaguzi uliofanyika hivi karibuni.

image

Alikamatwa baada ya kuandaa sherehe zake mwenyewe za kuapishwa kabla ya sherehe za kuapishwa kwa Rais Yoweri Museveni
aliyechaguliwa kwa muhula wa tano.

Kiongozi huyo amekuwa kizuizini muda mwingi tangu February mwaka huu. Rais Museveni amekanusha madai ya kuiba kura.

Ulinzi ulikuwa umeimarishwa kwenye sherehe za kuapishwa kwa Museveni Alhamis iliyopita ikiwa pamoja na kuzuiliwa kwa maandamano ya upinzani.

Serikali iliwaonya waandishi habari kutoripoti maandamano yoyote.

Mitandao ya kijamii kama vile Whatsapp, Facebook na Twitter
Ilizuiliwa kwa agizo la serikali ikidai ni sababu za kiusalama.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents