Tupo Nawe

Kipigo cha goli 2-0 cha Simba vs JS Sauora, Chamfanya Haji Manara abadili kauli mbiu ya klabu

Kufuatia kichapo cha goli 2-0 dhidi ya JS Saoura jana usiku, Msemaji wa klabu hiyo, Haji Manara amezungumzia hatma yao katika michuano hiyo ya klabu bingwa barani afrika.

Manara kupitia kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii, amesema kuwa kwa sasa ni ‘DO OR DIE’ akiimanisha ni kufa na kupona badala ya kauli mbiu yao ya ‘YES WE CAN’ ambayo wamekuwa wakiitumia kwenye michuano hiyo tangu mwanzoni mwa mashindano.

Ni Do or Die Match Ni zaidi ya Kufa au kupona Kwenye mchezo wetu wa mwisho dhidi ya AS Vita utakaochezwa Taifa Jumamosi ijayo!!
Bila kujali matokeo yatakayotokea Egypt baina ya Al Ahly na Soura ambao nao wanacheza siku hyo ya tarehe 16,ushindi wowote tutakaoupata dhidi ya Wacongo hao tutafuzu ktk Robo fainali!! Hiyo sio Yes We Can,hyo ni Do or Die kama ilivyokuwa na Nkana Insha’Allah itakuwa,
“.

Kwa sasa Simba SC wanaburuza mkia kwenye msimamo wa kundi D linaloongozwa na JS Saoura yenye alama 8.

Mchezo unaofuata Simba watacheza na AS Vita ya DR Congo, na ndio mchezo ambao Simba watahitaji ushindi wa namna yoyote ile ili wafuzu hatua inayofuata.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW