Aisee DSTV!

Kipigo cha mabao 2 – 1 dhidi ya Wolves champa mashaka Maurizio Sarri ‘Kiukweli nimejawa na hofu’

Meneja wa Chelsea, Maurizio Sarri amejikuta akishindwa kuelezea baada ya kupokea kipigo asichotarajia cha mabao 2 – 1 dhidi ya Wolverhampton Wanderers.

Maurizio Sarri admits he is 'very worried' after Chelsea slipped to defeat away at Wolves

Chelsea imejikuta ikipoteza  mechi yake ya pili sasa kwenye ligi hiyo huku ikiwa na kibarua kizito cha kuwakabili vinara wa ligi Manchester City wakiwa nyumbani Stamford Bridge Desemba 8 siku ya  Jumamosi.

Chelsea ambayo ilikuwa haijapoteza hata mechi moja ilianza kupoteza mbele ya Spurs kwenye dimba la Wembley kabla ya kukubali kipigo kingine hapo jana, Sarri amesema walikuwa wameutawala mchezo.

”Tulikuwa tumeutawala mchezo lakini baada ya goli lao la kwanza ghafla ilikuwa kama ajali, mara ghafla tunaangalia timu nyingine, tumecheza pasipokuwa katika pozisheni sahihi, pasipo mpira,” amesema Sarri.

”Kiukweli nimejawa na hofu, siyo kwaajili ya matokeo tuliyopata lakini ukweli ni kwamba hatukuweza kuonyesha kuguswa baada ya kutufunga bao la kwanza.”

”Tulikuwa na nafasi nne au tano hivi za kufunga magoli lakini tulishindwa kufanya hivyo, kisha tukapoteza kila kitu sifikirii kuwa ilitegemea na mabadiliko niliyofanya nadhani ni kutokana na uwezo wa kufikiria.”

Chelsea ikiwa na jumla ya pointi 31, ikishika nafasi nne itakuwa na kazi ya kufanya ili kuhakikisha inapata alama tatu mbele ya City wanaoongoza msukani wa ligi kuu EPL kwa kuwa na pointi 41.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW