Michezo

Kipigo cha Nadal chambakiza Murray viwango vya dunia

By  | 

Mcheza tenisi wa Uingereza, Andy Murray amesalia kuwa  namba moja katika viwango vya ubora wa mchezo huo duniani baada ya mpinzani wake Rafael Nadal kukubali kipigo kutoka kwa Denis Shapovalov siku ya Alhamisi.

Mcheza tenisi wa Uingereza, Andy Murray

Nadal aliitaji ushindi ili kutinga hatua ya Nusu Fainali ya michuano ya Montreal Masters na kumuondosha Murray katika nafasi hiyo hapo jana dhidi ya Shapovalov raia wa Canada mwenye umri wa miaka 18

Mchezaji tenisi, Rafael Nadal (kushoto) na  Denis Shapovalov (kulia)

Shapovalov ambaye anashika nafasi ya 143 katika viwango vya ubora duniani amejiwekea rikodi nzuri ya ushindi wa michuano hiyo ya Montreal kwa seti 3-6 6-4 7-6  baada ya kutumia saa mbili na dakika 45.

By Hamza Fumo

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments