Michezo

Kipigo cha Ruvu Shooting jana Masau Bwire atema cheche ‘Tunatuma salamu Jangwani, tutaitikisa Yanga’

Ligi kuu soka Tanzania Bara iliendelea hapo jana kwa michezo miwili kupigwa katika viwanja tofauti huku Ruvu Shooting ikikubali kipigo cha mabao 2 – 1 kutoka kwa Lipuli FC.

Mara baada ya matokeo hayo msemaji wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema kuwa kipigo hiko ni kama hitilafu kwenye usafiri wa ndege kwakuwa si rahisi kutokea kwake.

”Kilichotokea hapa ni hitilafu ya kawaida, huwa si rahisi ndege kupata hitilafu na inapotokea huwa ni hitilafu ambayo abiria wanataarifiwa mapema wanajua kweli kunahitilafu na sikawaida kutokea,” amesema Bwire.

Masau Bwire ameongeza ”Kilichotokea hapa ni hitilafu ya kawaida ambayo mara nyingi sikawaida kutokea, tumepoteza tumefungwa goli mbili la kwanza likipatikana kwa njia ya penati na kupata la pili kwa mabeki wetu kujichanganya tukamaliza hicho kipindi cha kwanza tukiwa nyuma kwa goli hizo mbili.”

”Vijana walipambana lakini bado ngome ya Lipuli FC ilisimama imara, kosa kosa zikawa nyingi golini mwao lakini Mungu hakutaka nyavuzao zitikiswe.”

”Vijana wamejipanga kutoa salamu pale Jangwani, unajua mchezo unaofuata tunacheza na Yanga na mimi naamini kwamba kitu kinapotokea huwa ni mipango ya Mungu, wakati fulani furahia kile unachokipata tukitumaini kwamba kinachokuja kinaweza kuwa bora kuliko hichi kilichotokea leo.”

”Ninahakika kwamba matokeo haya ya leo ambayo sisi kwetu yamekuwa mabaya ni chachu ya kufanya vyema katika mchezo unao kuja, tutakuwa Dar es salaam uwanja wa Taifa tarehe 16 tukicheza na Yanga tukihitaji walau tuitikise kidogo.”

Matokeo ya mechi mbili za leo yameendelea kuiweka Yanga kileleni huku Lipuli FC ikipanda kutoka nafasi ya 15 hadi nafasi ya 10.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents