Habari

Kipindupindu chamliza Meya Kinondoni, atoa somo kwa wanafunzi (Video)

Meya wa Manispaa ya Kinondoni Benjamini Sitta ametoa wito kwa watanzania wote kuzingatia umuhimu wa usafi hasa kwa kuzingatia zoezi la kunawa mikono kabla na baada ya kula au chochote kile ili kuweza kuepukana na baadhi ya magonjwa ambayo huwa ni rahisi kuepukika kwa urahisi.

Ameyasema hayo hivi leo wakati alipokuwa akifungua maadhimisho ya siku ya unawaji mikono Duniani maadhimisho ambayo yamefanyika katika shule ya msingi Kigogo iliyopo manispaa ya kinondoni Jijini Dar es salaam.

Aidha, ameongeza kuwa hivi sasa kumekuwa na ongezeko kubwa la baadhi ya magonjwa ambayo yanasababishwa na uchafu  , magonjwa ambayo  ni rahisi zaidi  kuepukika kwa kuafuata kanuni za usafi,huku akibainisha kuwa wazazi/walezi  husika ndio wanaopaswa kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha swala la afya kwa jamii,watoto,nyumba,au popote pale linazingatiwa na kuchukiliwa uzito kwani itasaidia pia katika kuondokana na baadhi ya magonjwa kama vile ya Kipindu pindu.

Sanjari na hayo meya Sitta amesema, baadhi ya watotozaidi ya milioni tatu na nusu hupoteza maisha kote duniani kwa kuugua Kipindu pindu huku watoto zaidi ya laki mbili katika jangwa la kusini mwa sahara hupoteza maisha huku katika manispaa  ya kinondoni katika kipindi cha hadi mwaka jana watoto walioripotiwa ni sita ambao wote wameripotiwa kupoteza maisha kwa kuugua Kipindu pindu.

Ameongeza kuwa imewekwa siku hii muhimu ya Unawaji wa mikono ili  kuimarisha na kuongeza ufanisi katika kutambua pamoja na kuelimisha zaidi baadhi ya matatizo ambayo huweza kusababishwa na kutozingatia usafi hasa wa kunawa mikono

Pamoja  na hayo Mhe. Sitta katika hotuba yake ameahidi kuijengea kisima kimoja shule ya msingi  mkwawa  ilyopo kigogoo , ili kuwezesha kuchangia katika upatikanaji wa majisafi shuleni hapo   ili kudumisha usafi na  kuepukana na adha ya uchafu na  changamoto  za ukosefu wa maji zilizopo kwenye baadhi ya shule  jambo ambalo hupelekea wanafunzi kuwawachafu hasamikono wanapotoka  msalani.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents