Habari

Kisa cha wana ndoa waliofariki pamoja chashangaza wengi

By  | 

Wanandoa Isaac Vatkin (91) na mkewe Teresa (89) waliofunga ndoa miaka 69 iliyopita wameishangaza dunia baada ya kufariki wakiwa wameachana kwa saa moja pekee.


Isaac Vatkin na Teressa enzi za uhai wao

Wawili hao, ambao walikuwa wakiishi katika eneo la Illinois mjini Chicago, walifariki Jumamosi iliyopita. Inadaiwa kuwa Teressa ndiye alikuwa wa kwanza kufariki dunia kwa ugonjwa wa Alzheimers, ambapo wote wawili walikuwa wakipata matibabu katika hospitali ya Highland Park Hospital.

Wakati Teressa anafariki dunia, mumewe Vatkin alikuwa amemshika mkono akiwa katika kitanda kilichokuwepo jirani na kile alicholala mkewe. Kwa mujibu wa wauguzi katika hospitali hiyo, dakika 40 baadae Issac alifariki dunia kwa tatizo la kushindwa kupumua vizuri.


Picha ya Isaac Vatkin na mkewe Teressa wakati wa ndoa yao

Clara Gesklin ambaye ni mtoto wa wazee hao, ameiambia Daily Mail, “Upendo baina yao ulikuwa mkubwa sana, mmoja asingeweza kuishi bila mwenzake.”

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments