BurudaniMitindo

Kisura wa Tz Yarudi tena

 

Msako wa kumpata Kisura wa Tanzania mwaka2010/11, unatarajiwa kufanyika mapema Desemba11 mwaka huu.


Juliana Urio, Mwenyekiti  na mwanzilishi wa Kampuni ya Beautiful Tanzania Agency (BTA) leo aliongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salam na kusema kuwa  hii ni mara ya tatu kufanyika kwa mchakato huu, tangu ulivyoanzishwa mwaka 2007  na untarajia kuanza usahili mkoa wa Mwanza.

Pia itahusisha mikoa ile ya Mara, Shinyanga, Kagera, Tabora, Dar es Salaam , Arusha , Karatu, Dodoma , Iringa Mbeya pamoja na Songea.

Juliana alisema kuwa timu nzima ya  BTA ikiambatana na mwanamitindo chipukizi Kemmy Kalikawe wanatarajia kuondoka jijini Dar es Salaam mnamo Desemba 10 kwenda Mwanza kuanza zoezi hilo.
.
Aliongezea kwa kusema mchujo huo utazingatia vigezo vya wasichana  wenye sifa  za urefu sentimita 174, upana 36, kiuno 27, kifua 36 na umri kati ya miaka 18-27. Wasichana hao watakaoshiriki kwenye mchujo pia watapewa mafunzo juu ya janga la UKIMWI.

Taji la Kisura wa Tanzania kwa sasa linashikiliwa na Diana Ibrahim kutoka mkoa wa Mara ambapo fainali za mashindano haya yanatarajiwa kufanyika Machi 2011 na kumpata kisura wa kurithi taji hilo.

Juliana aliongezea kwa kusema shindano zima linahusha kumtafuta mwakilishi ( Model) ambaye ataiwakilisha nchi yetu ndani na nje vilevile ikiwa lengo kuu  la shindano la kisura wa Tanzania ni kuwajengea uwezo watoto wa kike kwenye kiwango cha uelewa na kujitambua katika mabadiliko ya tabia, na kuwapa elimu ya mfumo rasmi na ile isiyo ya mfumo rasmi.

Pia timu itawapa mafunzo ya ujasiriamali na mabadiliko katika maisha yao na kwa taifa zima kwa ujumla.

Shindano hili  la Kisura wa Tanzania limedhaminiwa na Family Health International(FHI), TBC1, Kiromo View Resort Hotel, TanFoam(Arusha, Hugo Domingo BASATA pamoja na GRM Prroduction

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents