Habari

Kituo cha Haki za Binadamu chaanika madudu yaliyojitokeza uchaguzi mdogo wa madiwani

Kituo cha Haki za Binadamu (LHRC), kimetoa tathimini ya ukiukwaji wa haki za binadamu katika uchaguzi mdogo wa madiwani wa marudio uliofanyika Novemba 26 mwaka huu uliofanyika katika Kata 43 zilizopo katika Halmashauri takribani 36 kwenye Mikoa 19.

Akizungumza na Waandishi wa habari leo, Naibu Mkurugenzi wa Kituo hicho, Bi. Anna Henga amesema kuwa pamoja na kwamba baadhi ya Kata uchaguzi umefanyika kwa uhuru na haki lakini lakini kituo hicho kimebaini uwepo wa uvunjifu mkubwa wa Haki za Binadamu pamoja na taratibu zinazosimamia uchaguzi nchini Tanzania.

Aidha Bi.Anna amesema kuwa kumekuwa na vitendo matumizi mabaya ya vyombo vya dola, matukio ya watu kutekwa na watu wasiojulikana, watu kupigwa, kukamatwa na kujeruhiwa kwa lengo la kuharibu na kuvuruga uchaguzi na kuwatia hofu wapiga kura.

Katika hatua nyingine, Kituo hicho kimetahadharisha kwamba matukio hayo yasipokemewa na jamii nzima ni kiashiria kibaya cha msingi mbaya utakao athiri chaguzi zijazo ikiwemo uchaguzi wa serikali za Mitaa wa mwaka 2019 na uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents