Habari

Kituo cha nyuklia kusaidia kutoa taarifa JWTZ

KITUO cha kutambua nguvu za nyuklia duniani kiitwacho RN64 kilichopo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kitalisaidia Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa kulipa taarifa za majaribio ya nyuklia kutoka pembe zote za dunia

Mwandishi Wa Habari Leo

 

KITUO cha kutambua nguvu za nyuklia duniani kiitwacho RN64 kilichopo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kitalisaidia Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa kulipa taarifa za majaribio ya nyuklia kutoka pembe zote za dunia hivyo kuongeza ufanisi wa JWTZ ikiwa ni pamoja na kujihami.

 

Msimamizi wa kituo hicho kilichogharimu zaidi ya Sh milioni 520, Felician Bundala alisema Dar es Salaam jana kuwa kituo hicho kitakuwa na manufaa makubwa kwenye suala la ulinzi wa nchi kwa kuwa kitaisadia pia JWTZ kutekeleza mikakati ya kujihami. Bundala alisema kwa kuwa kituo hicho kina uwezo wa kutambua majaribio ya nyuklia yakifanyika popote duniani, JWTZ itapata taarifa hizo haraka na kwa usahihi zaidi.

 

“Hata walipofanya juzi kule Korea (Kaskazini) sisi tulifahamu. Kitatusaidia hata kujihami, hata jirani zetu wakifanya majaribio tutafahamu,” alisema Bundala. Alisema kupitia taarifa za kituo hicho kilichojengwa na Shirika la Kimataifa Linalosimamia Matumizi ya Nguvu za Nyuklia (CTBTO), Tume Inayosimamia Matumizi ya Nguvu za Nyuklia Tanzania (TAEC) itaishauri serikali ikiwamo JWTZ kulingana na taarifa zitakazopatikana.

 

Source: Habari Leo

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents