Uncategorized

Kiungo wa Juventus Emre Can amtetea Ronaldo ” Sisi sio Wanawake huu ni mpira”

Kiungo wa Juventus Emre Can amtetea Ronaldo " Sisi sio wanawake huu ni mpira"

Kiungo wa klabu ya Juventus na timu ya taifa ya Ujerumani Emre Can amefunguka na kulalamikia adhabu aliyepewa mshambuliaji wa klabu hiyo kutoka mitaa ya Turin Cristiano Ronaldo. Can amefunguka na kuyalalamikia maamuzi ya mwamuzi wa mchezo huo kwani aliamua kumuonyesha Ronaldo kadi nyekundi mnamo dakika ya 29 ya mchezo.

Emre ameweza kujibu kwa kushangaza baada ya mwamuzi wa mchezo huo dhidi ya Valencia kumuonyesha kadi nyekundu Cristiano Ronaldo ambapo Can amesema hicho kitendokimeonyesha  kuathiri upungufu mkubwa katika maamuzi yake.

Ronaldo, ambaye aliisaidia timu yake akifunga magoli mawili kwa mara ya kwanza kwenye ligi akiitumikia timu yake ya Juventus mwishoni mwa wiki, mchezo wa usiku UEFA ndio ulikuwa wa Ronaldo kuonyesha uwezo wake aliouonyesha mwishoni mwa wiki kwa kupachika mabao mawili lakini kitendo cha jana kilisababisha Ronaldo kuweza kububujikwa na machozi, kwani ilionesha dhahiri ni maamuzi yaliyomuumiza sana.

Lkini pia dada yake Ronaldo anayejulikana kwa jina la Katia aliyalalamikia maamuzi ya refa huyo na alidai kwamba ” kuna nguvu katika kazi,hicho kitendo ni kujaribu kumharibia ndugu yake na sio vinginevyo”

Kwa upande wa Can aliongeza “Hiyo haikupaswa kuwa kadi nyekundu!” Alisema wakati akiongea na kipindi cha  soka kutoka DAZN. “Nilisikia tu refa akisema kwamba ni kwa sababu ya kuvuta nywele, lakini tutambue Sisi siyo wanawake, tunacheza soka na tunapaswa kutumia nguvu”

“Ikiwa unatoa hiyo kama kadi nyekundu, unaweza kutumia kama ni faulu tu, kwa silimia Mia moja , hiyo siyo kadi nyekundu na haikustahili kuwa kadi nyekundu “

Juventus wamebakiza michezo mitano katika michuano ya UEFA michezo miwili dhidi ya Manchester United pia michezo miwili dhidi ya Young boys na mchezo mmoja dhidi ya Valencia,na endapo kamati ya nidhamu ya UEFA itachukulia kitendo hicho cha Ronaldo kama ilikuwa makusudi basi ataikosa michezo mitatu na kama itachukuliwa kama ilikuwa bahati mbaya basi Ronaldo ataukosa mchezo mmoja.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents