Habari

Kiungo wa klabu ya Chelsea apata ajali ya gari (+Picha)

Kiungo wa klabu ya Chelsea, Mfaransa Tiemoue Bakayoko amepata ajali mbaya ya gari jana jioni katika eneo la Blundel Lane wakati akitoka mazoezini akirudi nyumbani.

Tiemoue Bakayoko

Bakayoko (23) alipata ajali hiyo dakika 5 baada ya kutoka mazoezini akiwa na gari yake aina ya Mercedes Benz G63 AMG SUV baada ya kuyumba na kuacha njia.

Hata hivyo, kaka wa mchezaji huyo ajulikanaye kwa jina la Namory amesema Bakayoko hajaumia sana kwenye ajali hiyo.

Namory amesema kuwa walikuwa wote kwenye gari na alimuachia Bakayoko aendeshe lakini baadae akamuona akishindwa kuliongoza gari kwa kukosa uzoefu kutokana na sheria za Uingereza kuendesha upande wa kushoto wa barabara ndipo akaacha njia na kuingia mtaroni.

Aliniambia anataka kuendesha mwenyewe ingawaje alijua fika ni hana uzoefu wa kuendesha kwa upande wa kushoto wa barabara kama alivyozoea nyumbani (Ufaransa), basi gari likamshinda akaingia mtaroni,“amesema Namory kwenye mahojiano yake na Sky Sport.

Bakayoko alijiunga na klabu ya Chelsea akitokea AS Monaco kwa dau la Euro milioni 40 na mpaka sasa amecheza mechi sita akiwa na Chelsea na kufunga goli moja.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents