Aisee DSTV!
SwahiliFix

Kiungo wa Leicester City James Maddison aendelea kuiumiza kichwa Manchester United

Kiungo wa Leicester City James Maddison aendelea kuiumiza kichwa Manchester United

Manchester City inataka kumpatia mshambuliaji wa England Raheem Sterling mkataba mpya – chini ya miezi 12 baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 kutia saini mkataba mpya . (Metro)

Mshambuliaji wa Barcelona na Argentina Lionel Messi, 32, anasema kwamba baadhi ya watu katika klabu hiyo hawamtaki mshambuliaji wa Brazil Neymar, 27, kurudi. (Metro 95.1 via Sun)

Manchester United wanafikiria kumsajili aliyekuwa kiungo wa kati wa Liverpool Emre Can. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 na raia wa Ujerumani alijiunga na Juventus 2018. (Sky Sports)

Mchezaji bora duniani Lionel Messi

United pia wana hamu ya kumsajili kiungo wa kati wa Leicester na England James Maddison, 22, mbali na mshambuliaji wa Lyon na Ufaransa Moussa Dembele. (ESPN)

Liverpool na Chelsea zinamtaka kiungo wa kati wa Bournemouth mwenye umri wa miaka 22 Lewis Cook. (Mail)

Mshambuliaji wa Paris St-Germain na Uruguay Edinson Cavani, 32, amekataa ofa ya kujiunga na klabu ya David Beckham ya Inter Miami . (L’Equipe via Calciomercato – in Italian)

James Madisson wa Liecester

Kiungo wa kati wa Arsenal Mesut Ozil anaamini amefanywa kisingizio katika klabu hiyo. Raia huyo wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 31 anasema kwamba atasalia katika klabu hiyo hadi mwisho wa kandarasi yake 2021.. (Times via The Athletic – subscription required)

Newcastle imeanza mazungumzo na ndugu wawili Sean Longstaff, 21, na nduguye Matty, 19, katika harakati za kukubaliana mkataba ili kuwaweka wawili hao katika klabu hiyo licha ya hamu kutoka kwa Man United . (Express)

Beki wa Crystal Palace na England Gary Cahill, 33, amesema kwamba kustaafu sio lengo lake baada ya kutochezeshwa akiwa katika klabu ya Chelsea msimu uliopita. (Times – subscription required)

Kiungo wa kati wa Arsenal Mesut Ozil

Mkufunzi wa zamani wa timu ya taifa ya Marekani Jurgen Klinsmann anatarajiwa kurudi katika ukufunzi wakati huu akiwa kocha wa timu ya taifa ya Ecuador. (Sun)

Rais wa klabu ya Napoli Aurelio de Laurentiis anasema kwamba klabu hiyo huenda ikalazimika kumuuza kiungo wa kati Kalidou Koulibaly. Manchester United ina hamu ya kumsajili mchezaji huyo wa Senegal mwenye umri wa miaka 28. (Talksport)

Manchester United iliwasilisha ombi la kumsajili beki wa Uturuki na Juventus mwenye umri wa miaka 21 Merih Demiral kabla ya kumsaini beki wa kati mwenye umri wa miaka 26 Harry Maguire. (Sky Italia via Sporx – in Turkish)

Khalidou KoulibalyHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Mshambuliaji wa Leicester City na Nigeria Kelechi Iheanacho, 23, huenda analengwa na klabu ya Besiktas. (Calciomercato – in Italian)

Mshambuliaji wa klabu ya Al-Sadd na Algeria Baghdad Bounedjah, 27, anachunguzwa na klabu ya Leeds , Lille na Marseille. (Le Buteur – in French)

Mkufunzi wa Leeds Marcelo Bielsa anasema kwamba angependa sana mshambuliaji wa Arsenal aliyepo kwa mkopo katika klabu hiyo Eddie Nketiah, 20, kufanikiwa katika klabu hiyo ya Elland .. (Yorkshire Evening Post)

Eddie Nketia

Beki wa Everton Lewis Gibson anataka kujiunga tena na Newcastle. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19 alikuwa shule ya mafunzo ya soka katika klabu hiyo ya Magpies. (Football Insider)

Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United, AC Milan, Inter Milan, Juventus na Paris St-Germain Zlatan Ibrahimovic, 38, ametoa ishara kwamba atstaafu kuichezea klabu ya LA Galaxy baada ya mechi yake wikendi hii (Sun)

Chanzo BBC.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW