Michezo

Kiungo wa Sampdoria ya Serie A, avua nguo na kubaki utupu uwanjani akishangilia bao

Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Sampdoria inayoshiriki ligi kuu ya nchini Italia Serie A, Riccardo Saponara ameonyesha staili ya  ahaina yake wakati akishangilia bao lake wakati wa mchezo wao wa dhidi ya Lazio.

Saponara mwenye umri wa miaka 26, baada ya bao hilo na kusherehekea kwa kuvua nguo na kubaki utupu amenukuliwa akisema kuwa kuna aina 99 za ushangiliaji.

Nyota huyo aliyefunga bao hilo dakika za nyongeza (90+9) ya mchezo lilisaidia mechi hiyo kumalizika kwa sare ya jumla ya mabao 2 – 2 katika uwanja wa Stadio Olimpico.

Kupitia mtandao wake wa instagram mchezaji huyo ameandika ”Ahsante kwa wachezaji wenzangu wote waliyoshirikiana na mimi katika kipindi hiki chaajabu hasa Lorenzo Tonelli.”

” Tulicheza vizuri kwenye kipindi cha kwanza lakini hatukufdanya vizuri na kupata bahati kwenye kipindi cha pili ambapo.”

Sampdoria ipo nafasi ya 11 ikiwa na jumla ya pointi 20 huku Juventus ikiongoza ligi hiyo ya Italia kwakujikusanyia alama 41.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents