Burudani

Kivuli cha penzi la Linah chaendelea kumtesa Amini, afunguka haya

By  | 

Muimbaji Amini amechukizwa na kauli za mashabiki katika mitandao ya kijamii kuuhusisha wimbo wake mpya ‘Yamoyoni’ kuwa amemuimbia aliyekuwa mpenzi wake wa zamani, Linah Sanga ambaye kwa sasa ni mjamzito.

Mashabiki hao kupitia mitandao ya kijamii wamekuwa wakidai muimbaji huyo bado analitamani penzi la Linah licha ya kuingia kwenye maisha ya ndoa.

Akiongea na Bongo5 Jumatatu hii, Amini amewataka mashabiki wa muziki wake kuelewa kwamba sio kweli kwamba wimbo ‘Yamoyoni’ alimuimbia Linah.

“Mashabiki wanatakiwa kujua mimi nafanya muziki kwa ajili yao, mimi nimepitia mahusiano na watu tofauti tofauti sio Linah tu. Kwahiyo huu wimbo sio kwaajili ya Linah mimi naimba kwaajili ya mashabiki wangu, ” alisema Amini.

“Tena Linah kwa sasa ana mimba ya mpenzi wake ambaye yupo naye hata mimi kwa sasa namaisha yangu. Mashabiki wanatakiwa kuangalia muziki na ujumbe sio kurudisha nyuma mambo yaliyopita ambayo hayana tija,”

Muimbaji huyo amewataka mashabiki wa muziki wake kukaa mkao wa kula kwaajili ya mambo mazuri huku akiwataka kuendelea kuusupport wimbo wake mpya ‘Yamoyoni’.

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments