Habari

KKKT lachangia milioni 240 kwa waathirika wa tetemeko la ardhi

Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),limechangia kiasi cha shilingi milioni mia mbili na arobaini kwa waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera.

dscf5020-800x600

Taarifa za kanisa kuchangia tetemeko zimetolewa na askofu mkuu wa kanisa hilo Dkt Fedrick Shoo,katika mkutano wa wachungaji wa kanisa hilo unaoendelea mjini Dodoma.

“Tulipopata taarifa za maafa yaliyotokana na tetemeko la ardhi kule Kagera, tumekusanya kiasi cha shilingi zipatazo milioni mia mbili na arobaini, kwaajili ya kuwasaidia wenzetu hao kutoka kwa wachungaji hawa waliopo hapa na maaskofu kutoka pia kwa washirika wetu wa nga’mbo,”, alisema Askofu Shoo.

Kwa upande mwingine, Askofu Shoo ameunga mkono juhudi za Rais Magufuli kuhamia Dodoma.

“Kutokana na azma hiyo ya mheshimiwa rais kuona makao makuu kweli yanahamia hapa, na sisi Kanisa la Kiinjili la Kirutheri tunayo nia ya kwamba tutahitaji kupata eneo katika makao maku hapa, mahali ambapo tutaweza kuweka pia taasisi zetu,” alisema.

Watu na taasisi mbalimbali wameendelea kuwachangia waathirika wa tetemeko hilo la ardhi.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents