Michezo

Klabu moja Premier League yapendekeza msimu wa ligi ukamalizikie China

Imeripotiwa kuwa moja ya klabu zinazo shiriki Premier League nchini Uingereza imetoa pendekezo kuwa mechi za ligi zilizo salia zihamishiwe China ili kukamilisha msimu.

Watendaji wa kuu wa klabu zote 20 zinazo shiriki Premier League wanatarajia kukutana mchena wa leo siku ya Ijumaa na kufanya kikao kwa njia ya video, hata hivyo wasi wasi umetanda kuwa huwenda wakashindwa kufikia muafaka juu ya njia sahihi ya kuokoa msimu wa ligi.

Akinukuliwa na mtandao wa Dail Mail, Mtendaji Mkuu wa klabu moja ya EPL amesema kuwa, “Nchi ambayo inapendekezwa sana ni China. Haileti maana, ni wazo lisilofaa kwa wakati huu na nafikiri litakataliwa. Kama tukiichukua ligi na kuipeleka sehemu nyingine duniani, ni wazi tutakuwa tumejimaliza“.

Afisa mwingine mkubwa wa klabu nyingine ya ligi amesema, “Ni kupoteza nguvu tu, sote tunatamani msimu urejee na tuendelee na maisha lakini ni Mungu tu ndiye anaweza kufanya maamuzi juu ya janga hili“.

One Premier League club has suggested the extreme idea of finishing the season out in China

Inadaiwa klabu hiyo ya premier league imependekeza mechi hizo kupelekwa umbali huo wa mile 5,000 kutoka ili tu kuhakikisha wanamaliza msimu.

Pendekezo hilo limekuja baada ya kuona China, ikiwa na matokeo mazuri katika vita dhidi ya virusi vya corona tangu janga hilo liliporipotiwa jijini Wuhan mwishoni mwa mwezi Disemba, hivyo kuonekana kama sehemu inayofaa zaidi.

Pendekezo hilo limetolewa kipindi hiki nchi hiyo ikiwa katika vita ya kupambana na virusi vya Corona ili kuisaidia EPL kutoufuta msimu wa ligi ambao utasababisha klabu kulipa Paundi Milioni 762 kwa makampuni ya haki za televisheni zilizolipa kwa ajili ya kuonesha mechi za msimu mzima.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents