Burudani ya Michezo Live

Klabu ya Chelsea imevujisha taarifa zikionyesha kiasi inavyowalipisha wachezaji wao kwa utovu wa nidhamu – Video

Klabu ya Chelsea imevujisha taarifa zikionyesha kiasi inavyowalipisha wachezaji wao kwa utovu wa nidhamu - Video

Orodha ya adhabu za mchezaji wa ndani kwa msimu huu zimevuja, zikionyesha jinsi wachezaji wanavyopigwa faini ya pauni 20,000 ikiwa wamechelewa kuanza mazoezi kwa wachezaji wa Klabu ya Chelsea kikosi cha Kwanza hutozwa kwa makosa mbali mbali ya ndani ya Klabu kwa msimu huu wa mwaka 2019/20

Katika orodha hiyo iliyotoka jana mitandaoni imeorodhesha jumla ya makosa 12 na faini zake (Kwa TZS)

1. Kuchelewa kwenye mechi au kukosekana wakati timu inaondoka – milioni 7.3

2. Kuchelewa kuripoti katika muda wa mazoezi – milioni 7.3 (Utalipa mara mbili kama utachelewa dakika 15 baada ya mazoezi kuanza)

3. Kuchelewa Gym – milioni 3
4. Kuchelewa matibabu – milioni 7.3

5. Kuchelewa vikao vya timu – milioni 1.4 kwa kila dakika moja.

6. Kuchelewa kuanza mazoezi – milioni 59

7. Simu kuita wakati wa mlo wa pamoja au Vikao – milioni 3

8. Kuripoti na mavazi yasiyo husika/sahihi kwa timu kusafiri au siku ya mchezo – milioni 3.

9. Kushindwa kuhudhuria mjadala wa Kocha baada ya mchezo, bila kutoa taarifa masaa 48 kabla kwa Meneja au Msaidizi wake – milioni 15.

10. Kukataa au kutofika kwenye shughuli za kijamii – milioni 15.

11. Kutotoa taarifa juu ya kuumwa au majeraha kabla ya siku kumalizika au Saa 1 na Nusu kabla ya mazoezi – milioni 29.

12. Kuchelewa kwenye ahadi ya vipimo vya afya – milioni 7.3

Faini zote zinatakiwa kulipwa siku 14 baada ya kutozwa, kinyume na hapo itakuwa mara mbili.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW