Michezo

Klabu ya Chelsea ya tenga pauni Mil 31 kumsajil beki Kostas Manolas

Klabu ya Chelsea ipo tayari kupeleka ofa ya uhamisho kwa beki wa kimataifa wa Ugiriki anayechezea katika klabu ya AS Roma ya Italia, Kostas Manolas.

manolas-e1428685167394

Manolas hadi saivi amesha cheza mechi 57 akiwa na klabu yake ya Roma tangu ajiunge na timu hiyo ya Serie A kutoka Olympiacos ya Ugiriki mwaka 2014, lakini sasa anahusishwa na kuhamia katika Premier League.

Gazeti la II Tempo limesema kuwa Chelsea inajiandaa kumpeleka Stamford Bridge beki huyo mwenye umri wa miaka 24 kwa dau la pauni milioni 31.4 mwishoni mwa msimu.

Roma chini ya kocha Luciano Spalletti inataka kumbakisha Manolas licha ya klabu kubwa barani Ulaya kupigana vikumbo kumuwania ikiwamo pia Arsenal.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents