Michezo

Klabu ya Cristiano Ronaldo yamtimua kocha wake siku tisa pekee toka kuingia kandarasi ya miaka mitatu

Iliyokuwa klabu ya mchezaji bora duniani, Cristiano Ronaldo Sporting Lisbon imemtimua kazi kocha wake Sinisa Mihajlovic baada ya kuitumikia timu hiyo kwa muda wa siku tisa pekee tangu kutangazwa kwake.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 49, raia wa Serbia aliingia mkataba wa miaka mitatu kabla ya rais wa klabu hiyo Bruno de Carvalho kupigiwa kura ya kuwachia ngazi ili kuiokoa timu hiyo iliyoingia kwenye machafuko baada ya wachezaji wake kuvamiwa na kundi la mashabiki mwezi Mei.

Mkataba wa Mihajlovic ulikuwa unamuwezesha kukusanya kitita cha pauni milioni 1.6 kwa msimu lakini kwa bahati mbaya dili hilo limeshindwa kwenda kama alivyotarajia.

Mara baada ya kuchukua madaraka rais mpya, Jose Sousa Cintra ndani ya klabu hiyo ameamua kuvunja mkataba na  Mihajlovic mbele ya vyombo vya habari hapo jana.

Timu ya Sporting ilimaliza nafasi ya tatu na kufanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya Europa League msimu uliyopita ndipo mashabiki wakavamia kwenye uwanja wa mazoezi na kufanya vurugu.

Mei 13 klabu ya Sporting ilipoteza mbele ya Maritimo na kumaliza nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ya Ureno na kukosa ubingwa siku mbili baadaye wachezaji na benchi zima likashambuliwa na mashabiki kwenye uwanja wa mazoezi na mchezaji mmoja kupata madhara.

Juni 23 rais Bruno de Carvalho akapigiwa kura ya kuachia madaraka ndani ya klabu hiyo na ndipo hapo jana siku ya Jumatano kocha huyo Mihajlovic akaachishwa kazi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents