Michezo

Klabu ya Mbeya City yapata kocha mpya raia wa Burundi

Klabu ya Mbeya City imefikia makubaliano na Kocha Nsanzurwimo Ramadhan kuwa kocha mkuu kwa mkataba wa awali wa msimu mmoja wa Ligi Kuu Tanzania Bara ‘VPL’ inayoendelea.


Kocha Ramadhan ni raia wa Burundi na anatarajia kujiunga na timu huko Kanda ya Ziwa inakoendelea na michezo ya Ligi kuu.

“Ramadhan ni coach mzuri. Anapenda sana tiki taka. Aliwahi kuwa coach wa Kiyovu Sport team ya hapa Rwanda. He likes entertaining football. All the best to Rama.” Maneno ya mchezaji mahiri wa zamani na Mwandishi wa habari Mwandamizi nchini Rwanda, Gakuba Abdul Djabar ‘Romaria’.

Kocha Ramadhani amewahi kuwa kocha kwa nyakati tofauti katika vilabu mbalimbali nchini Burundi, Rwanda, Botswana, Malawi, Uganda, na Afrika ya Kusini, pia amewahi kuwa mshauri wa ufundi katika timu ya taifa ya Burundi na kocha msaidizi/kocha mkuu wa Muda (care-taker) kwa timu ya taifa ya Malawi.

Hatua hiyo ni baada ya kuvunja mkataba wake na kocha Kinnah Phiri mwanzoni mwa msimu huu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents