Michezo

Klabu ya Simba imemtambulisha kocha wa makipa Mbrazil Milton

Klabu ya Simba imemtambulisha kocha wa makipa ambaye ni raia wa Brazil Milton. kupitia ukurasa wao wa Instagram wameandika ujumbe huu:-

Huyu ndio kocha wetu mpya wa makipa. Huyu ndio baba yetu katika milingoti mitatu ya Mabingwa wa nchi. Ndie mwenye jukumu la kuhakikisha makipa wetu wanakuwa bora maradufu.

Ni raia wa Brazil na jina lake ni Milton Nienov. Amewahi kuwa kocha wa makipa katika klabu za Polokwane City, Lamontville Golden Arrows FC, Super Eagles FC, Free State Stars FC za Afrika Kusini na Club de Regatas Vasco da Gama, Sport Club Recifie na Figueirense FC za Brazil.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents