Michezo

Klabu ya Simba wameamua kumtimua kocha wao Dylan Kerr

Uongozi wa klabu ya Simba umefikia uamuzi wa kuachana na kocha wake, Mkuu Muingereza Dylan Kerr pamoja na kocha wa makipa, Iddi Salim na sasa timu itakuwa chini ya Mganda, Jackson Mayanja.
Maamuzi hayo yamefikiwa katika kikao cha Kamati ya Utendaji kilichofanyika katika makao makuu ya klabu, Msimbazi, Dar es Salaam.

pickerr

Msemaji wa Simba SC, Hajji Sunday Manara amesema kwamba, klabu imevunja mikataba yake na makocha wote, Kerr na Mkenya Iddi Salim

Manara amesema kwa sasa Mayanja atakuwa na timu, huku mchakato wa kumpata kocha mkuu ukiendelea.
Kerr anaondoka Simba SC baada ya kuiongoza timu katika mechi 30 za mashindano yote tangu atue Julai kuchukua nafasi ya Mserbia, Goran Kopunovic akishinda 19, kufungwa tano na sare sita.
Na Kerr anafukuzwa baada ya Simba SC kutolewa katika Nusu Fainali Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar Jumapili, jambo ambalo limemfanya apoteze imani mbele ya uongozi.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents