Habari

Klabu ya Simba yaahirisha mazoezi yake kufuatia sakata la kutekwa Mo Dewij

Klabu ya Simba yaahirisha mazoezi yake kufuatia sakata la kutekwa Mo Dewij

Kufuatia kupotea kwa kiongozi wa klabu ya Simba na mmiliki wa kampuni ya Metl Mohamed Dewij alimaarufu Mo Dewij klabu ya Simba imeamua kuahirisha mazoezi yake.

Kupitia afisa msemaji wa klabu hiyo Haji Manara,ameandika katika ukurasa wake wa instagram kuwa “Uongozi wa klabu ya Simba kwa mashauriano na Benchi la Ufundi la klabu yetu,chini ya Kocha Mkuu Patrick Aussems limeamua kuhairisha mazoezi ya Timu leo,ili kutoa fursa kwa Wachezaji na Benchi la Ufundi kushiriki ipasavyo kwenye Dua na Sala kwa ajili ya kiongozi wetu MO..tunawaomba tena na tena watanzania na wanoitakia mema nchi yetu..wasiache kumuombea uhai na uzima Bwana Mohammed Dewji..Insha’Allah kheri
@moodewji 🙏🙏”

Kwani hadi asubuhi hii ya leo hakuna taarifa zozote zilizotolewa za kupatikana kwa kiongozi huyo mkubwa wa klabu ya Simba pamoja na mmiliki wa kampuni ya METL ambayo inafanya biashara zake katika baadhi ya nchi barani Afrika.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents