Michezo

Klabu ya Simba yamtambulisha rasmi kocha Joseph Omog

Uongozi wa klabu ya Simba, umemtangaza rasmi kocha Joseph Omog, kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo.

img_0078

Evans Elieza Aveva ambaye ni Rais wa klabu ya Simba, amemtangaza kocha huyo kutoka nchini Cameroon pamoja na kumsainisha mkataba wa miaka miwili ambao unamuwezesha kukinoa kikosi cha Wekundu Wa MSimbazi hadi mwaka 2018.

Omog amesaini mkataba huo jijini Dar es Salaam mbele ya waandishi wa habari.

Kocha huyo amerudi kwa mara ya pili kwenye ardhi ya Bongo na VPL baada ya awali kuifundisha klabu ya Azam FC na kufanikiwakuipa taji la ligi kuu kwa mara ya kwanza kwenye historia ya klabu hiyo msimu wa 2013-14

Omog amesema anaujua ukubwa wa Simba na changamoto zake na amesisitiza atapambana kuhakikisha kunakuwa na mabadiliko ingawa amesisitiza suala la muda kwa kuwa kila kitu hakiwezi kubadilika siku moja.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents