Michezo

Klabu ya Simba yawasili salama nchini Misri, Yapewa baraka na ubalozi wa Tanzania

Klabu ya Simba ambayo iliondoka jana usiku nchini Tanzania kuelekea Misri kwa ajili ya mechi ya marudiano na klabu ya Al-Masry kwenye mchezo wa kombe la Shirikisho, Klabu hiyo imewasili salama nchini humo.

Simba SC wametua mjini Port Said nchini Misri wakipitia Addis Ababa nchini Ethiopia, ambapo wakiwa huko wamekutana na balozi wa Tanzania nchini humo, Meja General Issa Suleiman Nassor na kupewa baraka zote.

Simba na Al-Masry walitoka sare ya goli 2-2 kwenye mchezo wa kwanza ambao ulipigwa hapa Tanzania na watahitaji ushindi kwa namna yoyote au sare ya kuanzia goli 3 ili waweze kusonga mbele.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents