Michezo
Klopp aanza kampeni za ubingwa wa EPL mapema, atua kambini na wachezaji 26 (+Picha)
Meneja wa klabu ya Liverpool, Jurgen Klopp akiwa sambamba na baadhi ya wachezaji wake wamewasili Melwood tayari kwa mazoezi ya mwanzo wa msimu wa ligi kuu nchini Uingereza.
Takribani wachezaji 26 wameonekana wakiwasili tayari kujiandaa na majukumu yanayo wakabili isipokuwa wale waliyoshiriki michuano ya kombe la dunia ambao bado wapo likizo.
Miongoni mwa wachezaji waliyo onekana kuwasili ni pamoja na James Milner na Danny Ings akiwa amempatia Adam Lallana ‘lift’.