AFCON 2019 Tupogo!
Vodacom Data Datani!

Klopp afunguka kuhusu Naby Keita ‘Uwezo wake haujafikia ule aliyokuwa nao RB Leipzig’

Meneja wa klabu ya Liverpool, Jurgen Kloop amesema kuwa mchezaji wake, Naby Keita bado hajafikia kiwango kile ambacho alikuwa nacho akiwa RB Leipzig lakini anaamini bado anauwezo na umuhimu mkubwa.

Kiungo huyo wakimataifa wa Guinea mwenye umri wa miaka 23, alianza dhidi ya Wolves Desemba 21 kati ya michezo yake nane ya Premier League aliyowahi kucheza huku Klopp akiamini kuwa anahitaji muda kujiamini.

Keita ni moja kati ya nyota wanne waliyosajiliwa na kwa wakati mmoja ndani ya kikosi cha Jurgen Klopp huku akiwa amekosa michezo mitatu mwanzoni mwa msimu kutokana na kusumbuliwa na majeraha.

Alipoulizwa kuhusu Keita amesema amezungumza naye na kilakitu kipo sawa.

“Hivyo ndivyo ilivyo, nimezungumza naye na kilakitu kipo sawa, ni kweli alikuwa bora zaidi Leipzig kwa hapa bado anajaribu kuzoea mazingira,’’ amesema Klopp.

“Kila mtu ameona mwanzoni mwa msimu namna alivyocheza. Amekuwa akisumbuliwa na majeraha ya hapa na pale.’’

Akimzungumzia Lallana Klopp amesema “Adam ni mchezaji ambaye siku zote anapenda kuwa anye, amekuwa na kiwango kizuzuri zaidi siku za hivi karibu tangu nilipomfahamu kipindi hiki amekuwa bora zaidi.’’Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW