Michezo

Klopp afunguka uwezo wa kikosi chake kabla ya kumkabili aliyekuwa nyota wake Philipe Countinho ‘Tumekuwa bora bila hata ya Coutinho’

Meneja wa klabu ya Liverpool, Jurgen Klopp amekiri kuwa hakutarajia timu hiyo ingeweza kuwa kwenye kiwango bora bila ya kuwepo aliyekuwa mchezaji wake Philippe Coutinho.

Picha inayohusiana

Mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Brazil aliondoka Anfield na kuelekea Barcelona mwezi Januari mwaka 2018 kwa dau la pauni milioni 146.

Sasa Coutinho anajiandaa kukutana na klabu yake ya zamani usiku wa leo kwenye dimba la Nou Camp kwenye mchezo wa nusu fainali wa michuano ya Champions League huku meneja wa Liverpool, Klopp akiamini kuwa timu zote ziko vizuri.

“Ndiyo tunamkumbuka Coutinho sana kwasababu alikuwa mchezaji wa daraja la juu katika dunia na nilipenda kufanya naye kazi. Lakini meshazoea kufanya kazi bila yeye, na tumekuwa tukifanya vizuri.” amesema Klopp.

“Wakati nilijua anahitaji kwenda Barcelona, sikufikiria kama tungeweza kuwa vizuri pasipo yeye, lakini tumefaniki katika hilo na imekuwa vizuri kwa pande zote.”

Liverpool itafanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali ya Champions League kama itapata matokeo mazuri kwenye dimba la Nou Camp.

Mechi kubwa inakuja ambayo ni nzito kwa upande wa Liverpool ambao wanalengo la kuhakikisha wanafanya vizuri na kwenye mbio za kuwania ubingwa wa Premier League kwenye mechi dhidi ya Newcastle.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents