Tupo Nawe

Klopp alia na rafu mbaya aliyochezewa Salah dhidi ya Man City

Jurgen Klopp anaamini nahodha wa Manchester City Vincent Kompany alifaa kupewa kadi nyekundu wakati wa mechi ambayo Liverpool walilazwa 2-1 uwanjani Etihad.

Kompany alionyeshwa tu kadi ya manjano kwa kumchezea visivyo mshambuliaji wa Liverpool kutoka Misri Mohamed Salah dakika ya 32.

Mchezaji huyo wa Ubelgiji alimkaba Mo Salah kwa kuruka miguu yake yote ikiwa hewani kana kwamba anateleza. Alimgonga Salah kwenye kifundo chake cha mguu.

Leroy Sane alifunga bao la ushindi dakika ya 72 na kupunguza uongozi wa Liverpool hadi alama nne.

Kompany aliondolewa uwanjani dakika ya 88 na nafasi yake akaingia Nicolas Otamendi.

“Nampenda sana Vincent Kompany lakini inakuwaje kwamba hiyo si kadi nyekundu?” Klopp alishangaa baada ya mechi.

“Ndiye mtu wa mwisho safu ya ulinzi anapomkabili. Akamgonga Mo vyema, basi hataweza kucheza tena msimu huu. Sio rahisi kwa mwamuzi na huenda hakuona nilivyoona mimi.”

Kompany alitofautiana na tathmini ya Klopp kuhusu tukio hilo lililotokea mambo yakiwa 0-0.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW