Michezo

Klopp apokea kwa masikitiko taarifa za Manchester City ”Namuonea huruma Pep Guardiola”

Jurgen Klopp amesema kuwa anamuonea huruma kocha mwenzake, Pep Guardiola pamoja na wachezaji wa Manchester City kwa kitendo cha kufungiwa na kutoshiriki michuano ya Uefa Champions League kwa kipindi cha muda wa miaka miwili.

Image result for 'I really feel for Pep and the players': Liverpool boss Jurgen Klopp comes out in SUPPORT of Guardiola and his Manchester City stars over their Champions League ban

Bosi huyo wa Liverpool amabye amemuacha mpinzani wake City kwa jumla ya pointi 25 kwenye msimamo wa Premier League baada ya kuibuka kwa goli 1 – 0 dhidi ya Norwich.

Klopp amesema kuwa ”Nafikkiria namna gani ilivyokuwa ngumu kwa wapenzi wa michezo, unawaamini watu wako,” lakini mwisho wa siku Uefa wanakuwa tofauti.

Image result for 'I really feel for Pep and the players': Liverpool boss Jurgen Klopp comes out in SUPPORT of Guardiola and his Manchester City stars over their Champions League ban

”Nilishituka mara nilipoona vichwa vya habari, nikiwa nimeona kwa uchache tu vikisema Manchester City lazima wakate rufaa. Wakati huo sikuwa na habari yoyote kwa kinachoendelea.” Amesema Klopp.

”Ukweli ni kwamba namuonea huruma sana Pep na wachezaji wake, kwa sababu hawajafanya kitu chochote kibaya hakika. Wao walikuwa wakicheza mpira tu, kwa vyovyote itakavyokuwa Pep amesaidia sana kuimarisha hii ligi lakini mwisho wa siku sote nilazima tuheshimu sheri.”

Manchester City imepigwa marufuku kushiriki katika ligi ya mabigwa Ulaya kwa misimu miwili ijayo baada ya kupatikana kwamba wamekiuka sheria za Uefa zinazoambatana na masuala ya fedha na leseni.

Bod ya udhibiti wa masuala ya fedha imesema City imevunja sheria kwa kuweka kiwango cha juu zaidi cha fedha katika mapato yake ya ufadhili kwenye mahesabu yake na katika ripoti ya fedha iliyowasilishwa kwa Uefa kati ya 2012 na 2016 ilionesha kwamba hawakupata hasara wala faida”, na kuongeza kwamba klabu hiyo haikutoa ushirikiano wakati wa uchunguzi”.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents