Michezo

Klopp: Mechi ya Liverpool na United ni mechi mama

Baada ya mechi za klabu bingwa Ulaya, leo na kesho ni zamu ya usiku wa UEFA europa league maarufu kama UEFA ndogo.

Jurgen-Klopp-1

Kwenye mashindano hayo vita kubwa usiku wa leo itakuwa kati Liverpool dhidi ya Manchester United, japo zinaonekana kusuasua kwenye ligi ya Uingereza lakini hawa ni wapinazani wakubwa sana.

Kuelekea mechi hiyo kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema Liverpool na United ni mechi mama.

Klopp alisema, “Siamini kwenye maadui wa mpira, naamini kwenye ujamaa wa kweli. Kiukweli sina tatizo na Van Gaal. Mechi kama hii ni mechi mama kwenye mpira wa miguu, mahasimu, timu zenye kushindana kwa muda mrefu.”

“Kila mtu anasoma na kusikia kuhusu United inawezekana wakawa na matatizo makubwa, mwaka mmoja nyuma sikuwahi kufikiria kuja kukaa kwenye benchi la Liverpool na kukutana na United kwenye ya ulaya,” aliongezea.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents