Burudani

Kocha Jose Mourinho atimuliwa Chelsea

Chelsea imemtimua meneja wake Jose Mourinho.

José Mourinho

Kocha huyo raia wa Ureno mwenye miaka 52, alikuwa akiifundisha Chelsea kwa awamu ya pili kuanzia June 2013.

Chelsea imekuwa na msimu mbaya zaidi kwa kufungwa mechi 16 hadi sasa.

Pep Guardiola, Guus Hiddink, Brendan Rodgers na Juande Ramos ni majina yanayotajwa zaidi kushika nafasi yake.

Akiwa na Chelsea, kocha huyo alishinda ubingwa wa ligi kuu ya England mara tatu, mbili katika awamu yake ya kwanza kati ya mwaka 2004 na 2007.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents