Kocha mnorway amwangia sifa Henry Joseph

Kocha mnorway amwangia sifa Henry Joseph
Kocha mkuu wa Kongsvinger ya Norway, Tom Nordlie anaamini nahodha wa
zamani wa timu ya Taifa na klabu ya Simba, Henry Joseph ataisaidia
klabu hiyo kufanya vizuri katika ligi

Henry alitambulishwa jana usiku mbele ya mashabiki elfu tano kwenye
uwanja wa Gjemselund kabla ya mchezo wa ugenini wa Ligi Daraja la
Kwanza dhidi ya Mjondalen IF siku ya Jumapili.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Tanzania amekabidhiwa jezi namba mbili(2)
na benchi la ufundi ikiwa ni wiki mbili tangu aliposaini mkataba
unakaompatia sh260m kwa mwaka.

Kocha Nordlie amesema kuwa Joseph ni mchezaji mzuri na umri wake unamwezesha kuichezea timu hiyo muda mrefu.

"Joseph ana uzoefu wa kimataifa kutokana na kuichezea Taifa Stars na
Simba katika michezo mingi na ameonyesha uwezo mkubwa wakati wa
majaribio yake."

Kocha huyo amesema kuwa kwa kushirikiana na wachezaji wengine, Joseph
atakuwa nguzo imara na hata waangusha katika ligi na watafanya vizuri.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wakala wa FIFA, Mehd Rhemtula,
alisema" kocha wake amesifu ujio wa kiungo huyo katika timu hiyo
utawapa nafasi wachezaji wengine kuiga uchezaji wake.

“Naamini yeye atakuwa mfano wa kuigwa kwa wachezaji wa Tanzania ambao
wanataka kucheza soka la kulipwa, ni mchezaji wa kiwango chake na
mwenye kipaji cha hali ya juu,” alisema Rhemtulla.

Alisema kuwa umri wa mchezaji unamruhusu kucheza kwa muda mrefu na kwa kiwango cha juu.

Aliwatoa wasiwasi wachezaji wa timu hiyo kuwa ujio wake hauwaathiri wachezaji wazawa wa timu hiyo kwani atatoa changamoto kubwa.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents