Michezo

Kocha mpya wa Man U, Van Gaal aanza vizuri kibarua chake, waiadhibu Angeles Galaxy 7-0

Kocha mpya wa Manchester United, Louis van Gaal ameanza vizuri kibarua chake cha kukinoa kikosi hicho baada ya kupata ushindi wa goli 7-0 dhidi ya Los Angeles Galaxy katika mchezo wa kirafiki uliochezwa nchini Marekani.

10513728_1647215502170193_285686536_n

Man U walionekana kucheza soka la kuelewana zaidi ambapo mpaka wanakwenda mapumziko walikuwa wakiongoza mabao matatu kwa sifuri.

927373_814184811949029_112595024_n

Katika kipindi cha pili Man United walionesha kubadilika kwa kiwango cha hali ya juu, ambapo walilishambulia lango la Los Angeles Galaxy na kufanikiwa kupata mabao mengine manne na hivyo kufikisha idadi ya mabao saba kwa sifuri mpaka dakika 90 zilipomalizika.

Mabao ya Man United katika mchezo huo ambao kwa saa za hapa nyumbani Afrika mashariki umechezwa majira ya alfajiri lakini kwa huko Marekani ilikua ni usiku, yamefungwa na Danny Welbeck huku Wayne Rooney, Reece James na Ashley Young wakifunga mabao mawili kila mmoja.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents