Michezo

Kocha Ubelgiji amshauri Lukaku kuondoka Manchester United

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ubelgiji Robert Martinez amemshauri mshambuliaji wa kikosi cha Manchester United Romelu Lukaku kuondoka ndani ya klabu hiyo na kwenda kutafuta changamoto nyingine katika klabu nyingne.

Lukaku ambaye alisajiliwa na Manchester United mwaka 20017 akitokea Everton na kuweza kufunga magoli 42 katika mechi 96 ameonekana kutokuwa katika mipango ya mwalimu Ole Gunnar Solskjaer kwa msimu ujao.

“nadhani saizi ni muda muafaka wa Lukaku kuondoka ndani ya United na kwenda sehemu nyingne kutafuta changamoto nyingine chini ya mwalimu mwingine”.

Martinez amewahi kumfundisha Lukaku katika ngazi ya klabu alipikuwa katika kikosi cha Everton na hadi sasa ni kocha wa kikosi cha Ubelgiji ambapo Lukaku ndio mfungaji bora wa mda wote.

Mwalimu solskjaer amemtoa katika mipango yake ya msimu ujao ndani ya United na nafasi yake ameonekana Rashford kuimudu vizuri na hivyo kukosa nafasi ndani ya United kwa msimu ujao.

By Edwini Haule

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents