Aisee DSTV!

Kocha wa Arsena Unai Emery afurahishwa na matokeo yao dhidi ya United “Hatukustahili Ushindi”

Kocha mkuu wa klabu ya Arsenal Mhispanyola Unai Emery amefunguka na kuweka wazi hisia zake na maoni yake katika mchezo wao wa jana dhidi ya Manchester United.

Mhispania huyo ameongea baada ya mchezo huo kumalizika katika uwanja wa Old Trafford ambapo matokeo yalikuwa ni sare ya magoli 2-2, ambako Arsenal walikuwa wa kwanza kuapata goli dakika ya 26 kabla ya Mfaransa Anthony Martial kusawazisha dakika ya 31, na mnamo dakika ya 68 Marcos Rojo wa United alijifunga goli baada ya Lacazzete kulazimisha mpira huo lakini goli hilo halikukaa sana kwani Jesse Lingard alisawazisha mnamo dakika moja mbele yani dakika ya 69 na kufanya matokeo yakawa 2-2.

Unai amewapongeza wachezaji wake na kusema amefurahishwa na matokeo kwani haikuwa kazi rahisi, Unai alisema

“Ninajivunia sana kwa kazi yetu nzuri tuliyoifanya na jinsi tulivyoitikia katika dakika zote 90, Tunapofanikiwa hili huwa ni wakati mzuri sana kwetu, lakini walisawazisha haraka sana ingawa tulicheza vizuri baada ya kupata magoli mawili,“Katika nusu ya pili, wachezaji wetu walifanya kazi nzuri ili kutafuta goli la ushindi, Nadhani tulikuwa karibu, zaidi yao, kutafuta goli la tatu lakini De Gea aliokoa zaidi ya mara mbili au tatu mashambulizi makali. “

Mbvali na Unai kuongea hayo pia Kiungo wa Arsenal Mnigeria Alex Iwobi aliongeza:-

“Tulijua kuwa itakuwa ni mchezo mgumu kwa sababu Old Trafford daima ni mahala pagumu sana kwa mgeni ” alisema kiungo huyo,“Nadhani ni vigumukuamini kwa sababu tulikuwa tayari mbele kwa goli mbili. Timu zote mbili zilipigana kwa bidii, hata hivyo, nadhani sare ni matokeo mazuri kwa timu zote mbili.”

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW