Michezo

Kocha wa Dortmund, Jurgen Klopp kuondoka mwisho wa msimu huu

Mtendaji mkuu wa klabu ya Borussia Dortmund, Hans Joachim Watzke amezungumza na vyombo vya habari na kudai kuwa walikubaliana mapema na kocha wa timu hiyo, Jurgen Klopp kusitisha mkataba wake mwisho wa msimu huu.

279839DA00000578-0-Klopp_was_alongside_chief_executive_Hans_Joachim_Watzke_left_and-a-7_1429123437475

Klopp mwenye umri wa miaka 47 ameitumikia klabu hiyo kwa kipindi cha miaka 7 na ameisaidia kupata ubingwa wa kombe la Bundesliga mara mbili, kombe la shirikisho na kuingia katika fainali ya kombe la mabingwa ulaya.

Klopp amesema kuwa kwa sasa anatazamia kupata kibarua katika klabu za ligi kuu ya Uingereza hasa kwenye klabu ya Manchester City ambayo amevutiwa nayo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents