Michezo

Kocha wa Gor Mahia, Dylan Kerr abwaga manyanga

Mwenyekiti wa klabu ya Gor Mahia, Ambrose Rachier amethibitisha kupata barua ya kuacha kazi kwa kocha mkuu wa timu hiyo, Dylan Kerr.

“Leo nimepokea barua ya kujiuzulu kutoka kwa kocha Dylan Kerr. Kwa niaba ya klabu, ninakubaliana na maamuzi ya kujiuzulu kwake kwa sababu amekuwa mtu mzuri kwetu hivyo nataka kumtakia kilalakheri,” amesema mwenyekiti huyo Rachier.

”Katika barua yake ya kujiuzulu ya tarehe 15 Novemba 2018, Kerr ameonyesha wazi kwamba atakuwa na nafasi nyingine ya kufundisha msimu mpya wa ligi na kuwashukuru viongozi wote wa klabu.”

Katika kusoma sehemu ya barua hiyo mwenyekiti amesema “Kwa huzuni kubwa nimeamua kukubali uwepo wa kocha mwingine ambaye ataweza kusaidi kumaliza msimu wa 2018/19.”

Na kuongezea “Nataka kuweka rekodi na kupenda kukushukuru mwenyekiti kwa kunipatia nafasi ya kufanya kazi na wewe na bora zaidi kwa klabu ya Gor Mahia FC.”

Kocha huyo aliwashukuru pia wachezaji wa Gor Mahia kwa kumpatia ushirikiano na kuwataka waweke mawazo yao katika kazi yao ya soka.

Kwa upande wake mwenyekiti wa klabu hiyo amemshukuru kwa kuiwezesha klabu hiyo kupiga hatu kutoka pale alipoikuta na kuongeza kuwa Kerr alikuwa kocha muelewa, mwenyeheshima na alikuwa mtu wa watu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents