Michezo

Kocha wa Man United Ole Gunnar, aanza kumchunguza mpinzani wake akimbia Ufaransa kuwashuhudia PSG wakipokea kipigo

Baada ya ushindi wa Man United wa 1-0 dhidi ya Leicester, Kocha wa Manchester United Mnorway Ole Gunnar Solskjaer alikwenda Lyon Ufaransa kutazama game ya PSG dhidi ya Olimpique Lyon iliyomalizika PSG wakipoteza 2-1.

PSG wanatarajia kucheza na Man United 16 bora ya UEFA Champions League mnamo tarehe 12 ya mwezi huu, Ingawa PSG watamkosa winga wao mahiri kutoka nchini Brazil Neymar Dos Santos kutokana na majeraha aliyoyapata.

Ushindi wa United dhidi ya Leicester umeiweka United katika nafasi nzuri kwani wamevuka hatua moja na kuwa nafasi ya 5 baada ya kukaa kwa muda mrefu kwenye nafasi ya 6.

Kwa sasa United wamepisha alama mbili na timu iliyo nafsi ya 4 ambayo ni Chelsea wakiwa na alama 50 huku United wakiwa na alama 48.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents