Michezo

Kocha wa Manchester United, David Moyes atwaa kombe la kwanza baada ya miaka 10

Kocha mpya wa Manchester United, David William Moyes jana ametwaa kombe la kwanza baada ya miaka 10 katika mechi ya kwanza ya ngao ya hisani dhidi ya Wigan Athletic katika uwanja wa Wembley, Uingereza.

640x426xdavid-moyes-wins-first-trophy.jpg.pagespeed.ic.exjWjIIUec

Manchester United ilipata magoli mawili kupitia mshambuliaji wake Robin van Persie na kuifanya Manchester kuibuka washindi dhidi ya Wigan. Ushindi huo umemfanya Moyes, kocha mpya wa Manchester kupata matumaini na kuwaondoa hofu mashabiki na wapenzi wa Manchester kuwa huenda akaweza kuimudu mikoba ya kocha wa zamani Sir Alex Ferguson.

Akitokea Everton, David Moyes alichaguliwa kuwa mrithi wa Sir Alex Ferguson. Alifanya vibaya katika mechi zake za majaribio na kuibua hofu kwa mashabiki na wapenzi wa Manchester kuwa hatoweza kukimudu kikosi hicho.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents