Tupo Nawe

Kocha wa Mbao FC atangazwa kuifundisha KMC ya Kinondoni

Aliyekuwa Kocha wa klabu ya Mbao FC ambaye ni raia wa Burundi, Ettiene Ndayiragije amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuifundisha KMC ya Manispaa ya Kinondoni ambayo imepanda kucheza ligi kuu msimu ujao.

Ettiene amesaini mkataba huo Ijumaa hii kwenye ofisi ya Meya wa Manispaa ya Kinondoni Benjamin Sitta zilizopo Jijini Dar es Salaam.

Mapema mwezi April mwaka huu kocha huyo alitajwa kutakiwa na Yanga kwa ajili ya kurithi mikoba ya George Lwandamina lakini dili hilo lilionekana kupotelea hewani.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW