Michezo

Kocha wa Togo amtema Adebayor kwenye timu ya taifa

Kocha wa timu ya taifa ya Togo, Tom Saintfiet, amesema hatomuita katika kikosi cha taifa mchezaji Emmanuel Adebayor.

Adebayo

Saintfeit amesema Adebayor, 31, alishindwa kujibu alipoitwa kwenda kucheza dhidi ya Djibouti Septemba 4.

Mwezi Juni, alitishia kutocheza baada ya kuvuliwa unahodha.

Saintfeit amesema hayo alipo ongea na waandishi wa habari.

“Kama una mpenzi ambaye anaonekana kusuasua, basi inabidi utafute mwingine,” alisema.

“Kwa mujibu wa Saintfeit, Adebayor alishindwa kutoa jibu lolote kwa utawala wa Togo kwa ujumbe mfupi au hata kwa barua pepe.

“Kwangu mimi, ni wazi kuwa ni mchezaji asiyetaka kuichezea tena timu yake ya taifa,” amesema Saintfeit.

Adebayor bado hajacheza mechi hata moja kwa Tottenham msimu huu na hajajumuishwa katika orodha ya wachezaji watakaocheza Ligi Kuu ya EPL na hata Europa.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents