Soka saa 24!

Kocha wa Yanga akerwa na sare ‘Nafasi aliyopoteza Makambo hata Mama yangu angeweza kufunga’

Kocha wa mabingwa wa kihistoria Ligi Kuu soka Tanzania Bara Yanga SC Mkongo, Mwinyi Zahera ameonyesha kukerwa na safu yake ya ushambuliaji hadi kufikia hatua ya kusema nafasi aliyopoteza mchezaji wake Makambo hata mama yake angeweza kufunga.

Zahera ameyasema hayo juu ya nyota wake, Heritier Makambo mara baada ya kumalizika kwa mchezo wao wa ligi kuu  dhidi Ndanda FC uliyokwenda sare ya bao 1 – 1.

“Kila mechi tunatengeneza nafasi, lakini kama washambuliaji hawafungi tutafanyaje?. Mfano nafasi aliyopoteza Makambo kwa kichwa, pale hata mama yangu angeweza kufunga,” amesema Zahera raia wa Kongo.

Huu ni mchezo wa pili kwa Yanga kutoa sare baada ya kufanya hivyo kwa Simba bila kufungwa mpaka sasa huku ikishika nafasi ya tatu sawa na mabingwa wa tetezi Simba wote wakiwa na alama 26 wakati vinara wa ligi Azam FC wakiwa na pointi 30.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW