Michezo

Kocha wa Yanga awajibu wanaohoji kuchoka kwa wachezaji kipindi cha pili ‘Hatuchezi na wanawake’

Kocha Mkuu wa mabingwa wa kihistoria ligi kuu soka Tanzania Bara Yanga SC, Mwinyi Zahera amewajibu wale wote wanaohoji sababu ya wachezaji wake kuonekana kuchoka na kuzidiwa kimchezo kila ifikapo dakika 45 za kipindi cha pili.

Kocha Mkuu wa Yanga, Zahera

Zahera ambaye ni raia wa Congo ameyasema hayo hapo jana mara baada ya kikosi chake kuibuka na ushindi wa jumla ya mabao 2 – 0 dhidi ya Singida United mchezo wa ligi kuu.

”Leo (jana) mimi naona ndiyo kama mechi ya kwanza uwezo wa wachezaji kuanzia beki hadi viungo wa kati uko vizuri na walikuwa na nidhamu ya hali ya juu,” amesema Zahera.

Zahera ameongeza ”Hii ni mechi ya kwanza, na Mtibwa hatukucheza hivi, mechi ya pili na yatatu hatukucheza hivi ila hii ya leo mimi naona kama wachezaji wamefanya kama jinsi tulivyopanga.”

”Wapo watu wengine wananipigia simu, tena wengine ni waandishi wa habari wananiandikia kocha kwa nini timu yako kipindi chapili mnaonekana kuchoka?, fahamu hatuchezi na wanawake tunacheza na wanaume mnaskia.”

Kocha huyo ambaye ameonekana akizungumza kwa msisitizo ameongeza kuwa ”Kocha si alisema hapa kwenye kikao tulicho maliza ligi nguvu sana (ushindani), na ukiangalia mechi zote tulicheza Mtibwa, Stand, Coastal,kila mchezo tumefunga goli kipindi cha kwanza sasa kipindi cha pili ugumu unaongezeka hatuchezi na wanawake tunacheza na wanaume wao wanakuja na sisi tunahitaji kufunga wanacheza vizuri.”

”Siyo sababu sisi jina letu ni Yanga basi ndiyo tutakuwa tunafunga tu hapana tunacheza na wanaume, tatizo moja la kisaikolojia unapofunga goli moja unakuwa unatetemeka na wenzenu nao ndiyo wanasema hapa hapa. Mnashinda 4 – 1 na Stand mara 4 – 2 hiyo ndiyo saikolojia timu ile yenye magoli machache muda unavyozidi kwenda ndiyo inakuwa na nguvu ya kutaka kurudisha.”

”Nyinyi ndiyo mnasema wanachoka hapana hawachoki ni hiyo saikolojia ndiyo inakuwa inawasumbua sasa, nguvu na mwili unakuwa na uwoga mara khafla mabao yanafika 4 – 3 mwisho wa siku wachezaji wanaomba Mungu mchezo umalizike hata kwa matokeo hayo ya 4 – 3.”

Yanga imeanza ligi kuu kwa kuwafunga Mtibwa Sugar mabao 2 – 1, kisha ikaibuka na ushindi wa 4 – 3 mbele ya Stand United, huku wakipata ushindi mwembamba wa bao 1 – 0 dhidi ya Wagosi wa kaya Coastal Union ndipo hapo jana kwa mara ya kwanza ikapata alama tatu kwa Singida United toka kupanda daraja timu hiyo jumla ya goli 2 – 0.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents