MichezoUncategorized

Kocha wa Yanga adai hana cha kujifunza kutoka Simba

Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga, George Lwandamina amesema kwa sasa hataki kuangalia wala kuzungumzia timu nyingine zinazoshiriki ligi kuu Tanzania bara ikiwemo Simba kwa kile alichodai kuwa hana cha kujifunza kwani tayari amekinoa vya kutosha kikosi chake kwa ajili ya kutetea ubingwa msimu ujao.

Tokeo la picha la Lwandamina
Kocha wa Yanga, George Lwandamina katikati

Lwandamina amesema kuwa kwa sasa anaumiza kichwa kuhusu timu yake tu na siyo nyingine hii ni kutokana na homa ya mchezo wa ngao ya yamii utakaochezwa Agosti 23 mwaka huu.

“Nafanya kazi kwa Yanga, hivyo kutokana na hilo nimekuwa si mfuatiliaji wa mambo ya timu zingine ikiwemo Simba, Sisi tunaendelea kujiandaa vizuri kuhakikisha tunafanya vizuri msimu ujao, Nakumbuka msimu uliopita timu zote tulizokutana nazo kwenye ligi zilitusumbua sana, hakuna ambayo ilikuwa rahisi kwetu, lakini kikubwa ambacho naweza kusema ushirikiano ndio ulifanikisha tukawa mabingwa, hivyo basi tutahakikisha tunaiendeleza hali hiyo katika msimu unaotarajiwa kuanza hivi karibuniā€,amesema Lwandamina kwenye mahojiano yake na gazeti la Championi

Hata hivyo, Lwandamina amewaonya wapinzani wake kuwa msimu ujao atahakikisha anatembeza dozi zaidi ya msimu uliopita ili kutetea ubingwa.

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents